KIUNGO Maarouf Tchakei inaelezwa kuwa alikuwa anapigiwa hesabu na mabosi wa Simba ambao walikuwa wanahitaji saini yake.
Abdelhak Benchikha, kocha mkuu wa Simba alikuwa anatajwa kwamba alikuwa anakubali uwezo wa kiungo huyo baada yà kumuona katika Mapinduzi Cup 2024 akiwa na Singida Fountain Gate.
Licha ya mabosi Simba kupeleka ofa kuhitaji saini yake walipishana nayo Kwa kumkosa akitajwa kuuzwa Ihefu.
Januari 17 Simba ilimtambulisha kiungo mwingine wa kazi Edwin Balua ambaye alikuwa anacheza ndani ya Tanzania Prisons hivyo anakuwa kwenye changamoto mpya wakati ujao msimu wa 2023/24.