>

MSHAMBULIAJI WA KAZI NI MNYAMA

RASMI nyota  Freddy Michael Kouablan ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba atakuwa kwenye changamoto mpya baada ya kusaini dili la miaka miwili.

Kouablan raia wa Ivory Coast ana miaka 26. Alikuwa ndani ya Klabu ya Ligi kuu ya Zambia ya Green Eagles.

Rekodi zinaonyesha kuwa mshambuliaji huyo wa kazi ni mabao 14 na pasi za mabao alitengeneza 4 ndani ya Green Eagles ya huko Zambia.

Anaungana na Pa Omar Jobe ambaye alitambulishwa mapema ndani ya Simba January 15 wengine ni Babacar Sarr, Saleh Karabaka na Ladack Chasambi ambao ni wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Simba.