INAPOPATIKANA nafasi uwanjani ni muhimu kwa wachezaji kuitumia kwa umakini. Wapo wale ambao walishindwa kuonyesha uimara kila walipopata nafasi mwisho wakapoteza kila kitu.
Maisha ya mpira ni nafasi ya kucheza inapokosekana ni muhimu kwa wachezaji kuitafuta kwa kufanyia tathimini kile ambacho kinawafanya wawe benchi, hivyo tu.
Tunaona kwenye mechi za Mapinduzi 2024 kuna wachezaji waliopata nafasi za kucheza wakaonyesha viwango bora hivyo ni muhimu kuwa endelevu kwenye mechi zinazofuata.
Kuna wakati wapo wachezaji waliofanya vizuri kwenye Mapinduzi mashindano yalipoisha na ule ubora wao ukagota mwisho hivyo ni muda wa kufanyia kazi makosa yaliyopita.
Kila mmoja anatambua kwamba nafasi ya kucheza ni kitu muhimu hivyo ni muda wa kufanyia kazi makosa ambayo yalipita kwenye mechi zinazofuata ikiwa watapata nafasi.
Muda ni sasa kwa kila mchezaji kulinda uwezo wake na kujitoa kwenye mechi ambazo watazipata kwa kuwa nafasi ni chache na ushindani ni mkubwa uwanjani.
Kila la kheri kwenye mechi za ushindani ambazo wachezaji mnacheza na inaonekana kuwa kila mmoja anapambania kile anachokitafuta.
Hakuna ambaye hapendi matokeo mazuri ni muda wa kufanya kweli kwenye mechi zote na ule ubora usichuje baada ya Mapinduzi kugota mwisho kwenye mechi ambazo mtakuwa mnacheza kusaka ushindi uwanjani.
Nidhamu iwe msingi kwenye kila hatua huku wachezaji mkicheza kwa tahadhari kubwa na kulinda kila wakati.