ALI KAMWE: TUTAREJEA TUKIWA IMARA

OFISA Habari wa Yanga, Ali Kamwe ameweka wazi kuwa wanaamini kwamba watarejea kwenye mashindano ya Mapinduzi wakati mwingine wakiwa imara baada ya kupoteza nafasi ya kutwaa taji hilo 2024. Ipo wazi kwamba Yanga iliondolewa katika hatua ya robo fainali na APR kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali na wamerejea Bongo kwa maandalizi ya mechi za kitaifa na kimataifa.