>

MUDA WA KUFANYA KWELI AFCON

ULE muda wa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania kufanya kweli na kupata matokeo kwenye mechi za ushindani ni sasa kwa kuwa mashindano ya AFCON yapo mbele yao huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkubwa kwa timu zote.

Kwa namna ambavyo kila timu inahitaji ushindi imani kubwa hata kwa wachezaji wa Stars nao pia hesabu kubwa ni kupata ushindi.Kupitia makosa kwa mechi zilizopita basi ni muda wa kuyafanyia kazi makosa ili kuwa imara kwa mechi zote.

Ipo wazi kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo mazuri uwanjani na kwa kupambana inawezekana kwa timu kupata matokeo mazuri. Hivyo tu basi inatakiwa kuwa katika mechi zote.

Maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi ni muhimu kufuatwa pamoja na wachezaji kuongeza nidhamu kwenye mechi ambazo watacheza.

Hii itafanya makosa kupungua kwa upande wao pamoja na adhabu ya kadi za njano zisizo za lazima kwenye kupambania kombe ndani ya uwanja wakati wa kutafuta matokeo inawezekana na muda uliopo ni sasa.

Ushirikiano mkubwa kwenye kutafuta matokeo ni muhimu kuwepo kwa kuepuka kucheza kwa kutafuta rekodi binafsi kwa kuwa muda uliopo sio wa kutafuta rekodi binafsi bali timu kiujumla.

Kwa wale watakaoanza kikosi cha kwanza ama wale watakaokuwa benchi lengo ni moja kutafuta ushindi kwenye mchezo husika na kazi ifanyike kwa wakati ambao upo kwa sasa kila la kheri.

Januari 8 wachezaji wa Taifa Stars tayari wamewasili Ivory Coast kwenye mji wa San Pedro tayari kwa mashindano ya AFCON yanayotarajia kuanza Januari 13, 2024.