SIMBA YASHUSHA JEMBE JINGINE

RASMI Januari 6 2024 Simba imemtambulisha nyota mwingine mpya ambaye ni kiungo katika eneo la ukabaji.

Nyota huyo ni kutoka Senegal anaitwa Babacar Sarr ametua ndani ya Simba ikiwa ni ingizo jipya katika dirisha dogo.

Anakuwa nyota wa pili kutambulishwa baada ya kiungo Saleh Karabaka kutoka JKU kuwa wa kwanza kutambulishwa katika dirisha dogo ilikuwa Januari Mosi 2024.

Katika eneo la ukabaji anaungana na Fabrince Ngoma, Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.