AZAM YAACHANA NA MSHAMBULIAJI IDRIS MBOMBO

Klabu ya Azam FC imetangaza kuachana na mshambuliaji Idris Mbombo (27) raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa ya Azam FC kwenye mitandao ya kijamii imesema “Thank You Idris Mbombo”.

Mbombo alijiunga na Azam FC mnamo Julai 31 2021 akitokea El Gouna FC ya Misri.

Tetesi zinadai Mkongomani huyo amejiunga na klabu ya Nkana FC ya Zambia.