UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utaratibu wao ni uleule kwenye kuleta wachezaji wapya na watafanya utambulisho wa tofauti. Inatajwa kuwa kwa sasa Yanga ipo kwenye hesabu za kumalizana na mchezaji kwenye nafasi ya ushambuliaji kwa ajili ya kuanza changamoto mpya ndani ya kikosi hicho ambacho kimetinga hatua ya robo fainali Mapinduzi 2024.