INAELEZWA kuwa Edwin Balua ambaye ni winga yupo kwenye hesabu za kusjiliwa na mabosi wa Simba.
Kwa sasa kikosi cha Simba kimeweka kambi Zanzibar ambapo kinashiriki Mapinduzi Cup 2024 na leo Ijumaa kinatarajiwa kuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya APR.
Nyota huyo anatajwa kufikia kwenye hatua nzuri ya kusaini dili la miaka miwili kupata changamoto mpya ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Abdelhack Benchikha.
Tayari Simba imemtambulisha nyota mmoja kutoka JKU ambaye ni Saleh Karabanka akiwa kafunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya waajiri wake wa zamani JKU.
Kuhusu suala la usajili, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa utaratibu wa usajili ukikamilika watatambulisha wachezaji wao.