LEGEND MKUDE ASEPA NA TUZO

LEGEND Jonas Mkude alipewa kitambaa cha unahodha katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi 2024 dhidi ya KVZ.

Baada ya dakika 90 Januari 4 ubao ulisoma Yanga 0-0 KVZ wakigawana poiñti mojamoja ambapo Yanga inafikisha pointi 7 kibindoni.

Mkude alipewa tuzo ya mchezaji aliyeonesha mchezo wa kiungwana ambapo ni zawadi ya laki mbili alipata kutoka kwa wadhamini City College of Health huku Salum Athuman wa KVZ akisepa na tuzo ya mchezaji bora wa mechi akikomba laki tano kutoka kwa NIC Insurance.

Nyota mpya Augustine Okra alipata maumivu katika mchezo huo alikwama kuendelea ikiwa ni mchezo wake wa kwanza.