>

AZAM FC YASHUSHA MTAMBO MWINGINE WA KAZI

MATAJIRI wa Dar  Azam FC rasmi Desemba 31 wametangaza kufikia makubaliano na Klabu ya El Marreikh kwa ajili ya kumsajili kipa wao wa kimataifa wa Sudan, Mohamed Mustafa.

Kipa huyo amepewa dili la mkataba wa miezi sita ambapo atakuwa kwenye viunga vya Azam Complex kwa mkopo.

Kipa huyo anatarajiwa kuwa kwenye majukumu yake katika kikosi cha kwanza baada ya Ali Ahmada na Iddrisu Abdulai kuwa wanakabiliwa na majeraha kiasi cha kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

Ikumbukwe kwamba kwenye usajili wa dirisha dogo ni Franklin Navarro alianza kutambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Azam FC ilikuwa Desemba 28.

Tayari mchezaji huyo raia wa colombia amejiunga na timu Zanzibar ambapo yupo kwenye mipango ya Kocha Mkuu Yusuph Dabo kwenye Kombe la Mapinduzi.