>

AZAM FC WAFUNGA DESEMBA KIBABE

DESEMBA imekuwa bora kwa Azam FC baada ya tuzo kuelekea Azam Complex kutoka Kamati ya Tuzo ya Shirikisho là Mpira w Miguu Tanzania, (TFF).

Ni Kipre Junior amechaguliwa kuwa mchezaji bora aliwazidi Prince Dube wa Azam FC na Aziz KI wa Yànga.

Mbali na Kipre ambaye alihusika kàtika mabao manne kwenye michezo mitatu ndani ya dakika 235 kocha Bruno Ferry wa Azam FC ametwaa tuzo ya kocha bora.

Bruno kawazidi Miguel Gamondi wa Yanga na Ahmad Ally wa Prisons huku Meneja bora wa uwanja akiwa ni Amir Juma wa Azam Complex.

Hivyo Azam FC wamefunga Desemba 31 2023 kibabe wakisepa na tuzo zote Bongo ndani ya ligi.