Ndoto ya kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika ni ndoto ambayo klabu ya Simba wamekua wakiiota kila siku, Lakini ilionekana kuingia wasiwasi kutokana na mwanzo wao katika michuano hiyo msimu huu.
Baada ya ushindi wa mabao mawili kwa bila walioupata katika uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumanne umeibua matumaini upya kwa klabu hiyo, Kwani matumaini yalionekana kupotea na mashabiki wa klabu hiyo kuanza kufikiria huenda mwaka huu wasifuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.
Kufuzu hatua ya robo fainali kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwa klabu ya Simba hii imekua kawaida kwasasa, Hivo ndoto kubwa kwa klabu hiyo ni kutinga hatua ya nusu fainali lakini kwa namna timu hiyo ilipoanza michuano hiyo ni wazi matumaini ya kwenda nusu fainali yalififia.
Baada ya ujio wa kocha Abdelhak Benchikha ndani ya kikosi cha Simba ameonekana kufanya mabadiliko makubwa licha ya kukaa kwa kipindi kifupi, Hivo inaonekana kuna mambo mengi mazuri yanakuja chini ya kocha huyo mwenye Wasifu mkubwa barani Afrika.
Baada ya Wydad Casablanca kufungwa na Simba katika dmba la Benjamin Mkapa na Simba sasa klabu hiyo imebakiza michezo miwili ili kujihakikishia kufuzu katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika, Ambapo michezo hio itakua baina ya Asec Mimosas ugenini na mchezo wa mwisho nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Klabu ya Simba imejiwekea malengo ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika jambo ambalo wamekua wakilipigania kwa misimu takribani mitatu sasa, Japo msimu huu ilionekana kama wasingeweza kufuzu hata hatua ya robo fainali lakini ujio wa kocha Benchikha umeibua matumaini upya.
Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee
ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.