Home Sports KIMATAIFA KAZI KUBWA IFANYIKE KUSAKA MATOKEO

KIMATAIFA KAZI KUBWA IFANYIKE KUSAKA MATOKEO

MECHI ambazo zimebaki kwa wawakilishi wa kimataifa zote ni muhimu kushinda kufufua matumaini ya kutinga hatua ya makundi licha ya ugumu uliopo.

Kikubwa kwenye mechi za hatua ya makundi ni kuhakisha kwamba hakuna ambaye ataleta utani kwenye mechi ambazo zitachezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni mechi mbili ambazo zinamaana kubwa kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa ikiwa ni Yanga na Simba.

Kwenye mechi tatu ambazo zilipita hakuna ambacho kinaweza kubadilika kwa sasa zaidi ni kuangalia mechi tatu ambazo zinakuja kwa kuwa ni muhimu kupata ushindi.

Makosa ambayo yalifanyika hayo yanapaswa kufanyiwa kazi kwa umakini ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Wachezaji muhimu kujituma kwenye kukamilisha mpango kazi kutoka kwa benchi la ufundi na wakati mwingine pale mbinu zinapokwama hata zile binafsi nazo zinapaswa kutumiwa.

Kikubwa ni kuona ushindi unapatikana kwa kuwa mechi ambazo zimebaki hizi zitatoa picha ya nini ambacho kitaendelea kwenye hatua inayofuata.

Ikiwa timu zote mbili zitapata nafasi ya kusonga mbele mpaka hatua ya robo fainali itakuwa rekodi nzuri kwa timu zote mbili na kazi kimataifa itakuwa imefanyika kwa umakini.

Muda ambao wakufanya yote hayo yawe katika mwendo mzuri ni sasa na inawezekana kwa kila mchezaji kutimiza majukumu yake kwenye anga la kimataifa.

Kila la kheri wachezaji kwenye mechi zote na mashabiki pia mjitokeze kwa wingi kuwapa nguvu wachezaji kwenye mechi za nyumbani.

Previous articleBENCHIKHA ACHENI WAJE, MKATA UMEME MPYA AJA NA JAMBO
Next articleShaktar Donetsk Yahofia Kumpoteza Mtanzania Yamuweka Benchi