KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Farid Mussa yupo huru kusajiliwa na timu yoyote itakayohitaji saini yake ikiwemo Simba ambayo imepanga kukifanyia maboresho kikosi chake.
Hiyo ni kutokana na mkataba wake kufikia mwisho mwishoni mwa msimu huu akiwemo Chrispin Ngushi, Denis Nkane ambao hivi sasa wamepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
Kwa mujibu kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), mchezaji anaruhusiwa kufanya mazungumzo klabu nyingine mkataba wake ukiwabakiwa na miezi kabla ya kumalizika. Hivyo Farid yupo huru kwa sasa.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kiungo huyo anatajwa kuwindwa na baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, ikiwemo Singida Fountain Gate.
Mmoja wa Mabosi wa Yanga, ameliambia gazeti hili kuwa hadi hivi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa kati ya kiungo na uongozi wa timu hiyo kuhusu kuongeza mkataba mpya.
Aliongeza kuwa uongozi unafanya mazungumzo na wachezaji ambao wapo katika mipango ya kocha pekee, waliojihakikishia