KAGERA SUGAR KAMILI GADO KUIVAA SIMBA

BENCHI la ufundi la Kagera Sugar limebainisha kuwa linafanyia kazi makosa kwenye mechi zao zilizopita ili kupata matokeo katika mechi zijazo.

Mchezo wao ujao kwenye ligi ni dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Desemba 15 na kikosi hicho kinaendelea na mazoezi Uwanja wa Uhuru.

Marwa Chamberi, Kocha msaidizi wa Kagera Sugar amesema kuwa walipata muda wa kufanya mazoezi ligi iliposimama na kufanyia kazi makosa yao.

Wakati wa ligi iliposimama tulikuwa tunafanyia kazi makosa yetu tunaamini kwamba tutakuwa imara katika kupata matokeo kwani ushindani ni mkubwa hilo tunalitambua na wachezaji wapo tayari,”.

Mchezo uliopita Kagera Sugar ilipoteza ugenini kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.