>

KIMATAIFA KAZI KUBWA IFANYIKE, INAWEZEKANA

SIO Yanga wala Simba kwenye anga la kimataifa hakuna mwenye kazi nyepesi kutokana na mechi zao wote kuwa ngumu katika hatua ya makundi.

Tumeshuhudia namma mechi za kimataifa wapinzani walivyo wagumu na mechi ni ngumu. Hii inatokana na aina ya wachezaji pamoja na timu husika kuwa na mipango kazi ofauti na ile ambayo imezoeleka kwenye ligi ya ndani.

Michezo mitatu iliyobaki hii iwe ni zaidi ya fainali kwa kila timu kucheza kwa umakini kupata pointi tatu. Wakati uliopo ni sasa na inawezekana kushinda mechi zote tatu licha ya kwamba zina ugumu wake lakini furaha itakuwa kubwa ushindi ukipatikana.

Porojo kwa sasa hazipaswi kupewa kipaumbele bali ni vitendo zaidi katika dakika 90 za kusaka ushindi. Iwe ni kwa mechi za nyumbani pamoja na ugenini kwa kuwa mashindano ya kimataifa yanahitaji ushindi kila mechi kwa hatua ambazo Simba na Yanga zimefikia.

Mashabiki wa Tanzania wanapenda mpira na furaha yao ni kuona kwamba wawakilishi wao wanatinga hatua ya robo fainali. Muda ni sasa kwa kila timu kufanya kweli na inawezekana.

Mechi zilizobaki tatu kwa timu zote hakuna ambayo ni nyepesi iwe ni nyumbani ama ugenini kikubwa ni wachezaji kuchukua jukumu la kucheza mechi zote kwa kujituma kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kisha baadaye mipango ya nusu fainali itafuata.