KIUNGO wa Yanga Pacome Zouzoua amekuwa ni mwiba mkali kwa wapinzani kutokana na uwezo wake anaoonyesha ndani ya uwanja katika mechi za kimataifa.
Ikumbukwe kwamba Desemba 8 Yanga iligawana pointi mojamoja na Klabu ya Medeama kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo bao la Yanga lilifungwa na kiungo Pacome.
Hilo linakuwa ni bao la pili kwa Pacome kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuanza kufunga kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Desemba 10 Yanga iliwasili salama Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi zake zinazofuata ambapo ina mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar Desemba 16 unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.
“Kikubwa ni kuona kwamba timu inapata matokeo licha ya kushindwa kupata pointi tatu kwenye mechi yetu ya nyumbani bado tuna kazi ya kufanya kwenye mechi nyingine,”.
Baada ya kucheza mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga imekusanya pointi mbili katika kundi D ambalo wapo.