Home Sports AZAM FC YAIPIGA 5 G KMC, YASHIKILIA USUKANI

AZAM FC YAIPIGA 5 G KMC, YASHIKILIA USUKANI

MATAJIRI wa Dar Azam FC ni namba moja katika msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 13 wanafuatiwa na Yanga nafasi ya pili pointi 24 baada ya kucheza mechi 9.

Desemba 7 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 5-0 KMC.

Ni Prince Dube dakika ya 23 na 51 Ismail Gambo dakika ya 43 alijifunga, Gibril Sillah dakika ya 55 na Fei Toto dakika ya 60.

Ikumbukwe kwamba Azam FC mchezo wake uliopita wa kufungia Novemba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mtibwa Sugar haijawa kwenye mwendo mzuri mchezo wake wa Desemba 7 Uwanja wa Majaliwa ilishuhudia ubao ukisoma Namungo 1-0 Mtibwa Sugar.

Hivyo kwa sasa vinara wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 ni Azam FC yenye maskani yake Chamanzi, Dar.

Previous articleMAJEMBE YATAKAYOCHUKUA NAFASI YA MWAMBA LOMALISA
Next articleKIUNGO MGUMU KAANZA NA REKODI YAKE SIMBA