NI Feisal Salum nyota wa Azam FC amempoteza kiungo wa kazi ndani ya Yanga Maxi Nzengeli kwenye kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Novemba.
Fei ameibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba akiwapoteza Maxi Nzengeli wa Yanga na Kipre Jr. wa Azam FC ambao aliingia nao kwenye fainali.
Wakati Feisal aking’ara katika mwezi huo, kocha Bruno Ferry ameibuka kuwa kocha bora akiwashinda Miguel Gamondi wa Yanga na Heron Ricardo wa Singida Fountain Gate.
Kwa upande wa viwanja, aliyeibuka kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi huo, ni Nassor Makau wa CCM Mkwakwani, Tanga.
Hii ni kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za TFF na kutangazwa Desemba 5 2023.