KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Desemba 5 alfajiri kimeanza safari kuelekea Ghana kwa ajili ya kupambania kupata pointi tatu muhimu.
Baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 imekusanya pointi moja pekee.
Yanga inapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Medeama Desemba 8.
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Hafiz Konkoni, Mudathiri Yahya, Skudu Makudubela.
Ikumbukwe kwamba Yanga Desemba 2 ilishuka Uwanja wa Mkapa kumenyana na Al Ahly baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga 1-1 Al Ahly.
Bao la Pacome Zouzoah dakika ya 90 limechaguliwa kuwa bao bora la wiki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.