>

WAARABU WAMPA TUZO PACOME BONGO

LICHA ya kuambulia pointi moja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa bado Yanga hawakumaliza mechi hiyo kinyonge.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Desemba 2 na ubao ukasoma Yanga 1-1 Al Ahly ya Misri bao alilofunga nyota wa Yanga limebeba tuzo ya bao bora la wiki.

Ni Pacome Zouzoua alipachika bao la kuweka usawa dakika ya 90 ikiwa zimepita dakika nne tangu wafungwe bao la kwanza kwenye mchezo huo kipindi cha pili.

Waarabu hao wa Misri waliamini wanaweza kusepa na pointi tatu kabla ya Pacome kuwaduwaza dakika za jioni na bao lake akitumia mguu wa kulia lililopewa tuzo ya bao bora la wiki.

Ilikuwa ni kwenye mechi ya pili hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Pacome alifunga bao hilo lililowanyanyua mashabiki wa Yanga kwenye viti na kushangilia pointi moja.

Taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa rasmi wa CAF imeelezea kuhusu bao hilo na maeneo aliyokuwepo Pacome.

Katika ardhi ya Tanzania , katikati ya mabeki watatu, mechi ya pili bao la wiki kwa mashindano ya CAFLL linakwenda kwa Pacome Zouzoa wa Yanga,”