VURUGU KWA MASHABIKI MUDA WAKE UMEGOTA MWISHO

MASHABIKI ni muhimu kufika uwanjani kwa ajili ya kushangilia mechi ambazo zinachezwa lakini ni muhimu kuwa makini na kuacha kufanya vurugu kwenye mechi husika.

Afya ni muhimu kwa mashabiki ili kuendelea kusukuma gurudumu kwenye maisha ya kila siku. Ripoti za mashabiki kupigana ama kupigwa hazipendezi kuwa endelevu kwenye ulimwengu wa mpira.

Ukweli ni kwamba kila mmoja anatambua kuhusu ushindani ulivyo na namna ambavyo timu zinapambana kupata matokeo mazuri.

Kikubwa ni kuwa makini kwenye mechi zote za ushindani. Mashabiki wanapaswa kuwa na utulivu kwenye mechi zote na inawezekana kutokana na kuwa makini kwenye kushangilia timu zao.

Masuala ya kubeba matokeo kwenye mechi ambazo wanakwenda uwanjani ni muhimu kuziacha kwa kuwa mpira ni dakika 90.

Hakuna mchezo ambao unamatokeo kabla ya kuchezwa hivyo mashabiki ni muhimu kutambua kwamba hakuna anayetambua nani atashinda kwenye mchezo husika.

Wakati wa kuendelea kuwa bega kwa bega kwenye mechi ambazo wachezaji wanacheza na itaongeza nguvu kwa wachezaji kupata matokeo chanya uwanjani.

Muda ni sasa kwa kila mchezaji kutambua kwamba mashabiki wanapenda matokeo mazuri na hilo linawezekana kwa kila mchezaji kuongeza juhudi ndani ya uwanja.

Matokeo mabaya yanaumiza lakini haitoi ruhusa kwa mashabiki kupambana na kufanya jitihada kwa kuwapa furaha mashabiki na kucheza vizuri ndani ya uwanja kila mechi kwa kufuata sheria 17 za mpira.