Novemba 27 Kagere alifunga bao lake la kwanza kwenye ligi na wakati wa kushangilia alionyesha fulana iliyoandikwa, “Mnafiki ishi naye kinafiki,”.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo ambao Singida Fountain Gate ilishinda kwa mabao 2-1 Coastal Union Kagere alisema.
“Maisha ya duniani tunaisha kinafiki tunaishi hivyo lakini sisi wote tukisihi kwa umoja bila kuonyesha unafiki kwa umoja itakuwa vizuri
“Tunaishi na watu ambao wanacheka lakini hawana ushirikiano. Niujumbe wangu ambao unakwenda na kazi ambayo ninafanya na namna ya ushangiliaji lakini ninamshukuru Mungu.
“Sio rahisi unakuwa umekosa kupata nafasi ya kucheza kwa muda unapata majibu kwa kufunga kwenye mechi hivyo ni furaha kwamba nimefungua namna ya kupata ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza,”.
Ni ushindi wa kwanza kwa Singida Fountain Gate kuupata wakiwa Uwanja wa Liti kwa msimu wa 2023/24.