HUYU HAPA KOCHA MPYA SIMBA

Klabu ya Simba imemtangaza ABDELHAK BENCHIKHA kuwa kocha mkuu klabuni hapo akichukua mikoba ya Robert Oliveira ‘Robertinho’ aliyeoneshwa mlango wa kutokea.

Benchikha (60) raia wa Algeria aliiongoza USM Alger kuwaa kombe la Shirikisho Afrika kwa faida ya magoli ya ugenini dhidi ya Young Africans SC kwenye fainali.

Benchikha pia aliiongoza USM Alger kutwaa CAF Super Cup kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo baada ya kuifunga Al Ahly 1-0 kabla ya kujiuzulu nafasi yake klabuni hapo mnamo Oktoba 9, 2023.