>

KOCHA MPYA SIMBA ANALITAMBUA SOKA LA AFRIKA

KLABU ya Simba imemtangaza Abdelhak Benchikha raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 60 kuwa kocha wao mkuu.

Kocha huyo anarithi mikoba ya Roberto Oliveira, ( Robertinho) ambaye alisitishiwa mkataba wake muda mfupi baada ya kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.

Kocha huyo ana uzoefu mkubwa kwenye mechi za ushindani hivyo wachezaji wa Simba wakiwa naye sawa wanaweza kuwa kwenye mwendo tofauti.

Ni uzoefu wa kufundisha nchi za Africa kama vile:- USM Algers,  ES Setif, CR Belouizdad, MC Algers,  ES Zarzis, CABB Arreridj hizi ni za Algeria pia alifanya kazi nchini Morocco akiinoa RS Berkane, Raja Athlethic,  Difaa El Jadida, Mouloudia, Ittihad Tnager, Moghreb Tetounan.

Tunisia ni Club Africain aliwahi kuinoa timu hiyo kwenye mechi za ushindani na mashindano mbalimbali.

Rekodi zinaonyesha kuwa ni jumla ya mechi 377 kaziongoza huku akiambulia ushindi kwenye mechi 134, sare 112
aliambulia kichapo kwenye mechi  131.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 alitwaa taji la Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na Klabu ya USM Alger na alpata ushindi dhidi ya Yanga kwa faida ya bao la nyumbani kwa kuwa mchezo wa fainali ya pili alipoteza na Yanga walicheza mpira mzuri ugenini.

Vyanzo

– TransferMarkt
– Football Database
– Sofascore