IHEFU YAACHA POINTI TATU KWA NAMUNGO

KLABU ya Ihefu ikiwa ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo iliacha pointi tatu baada ya dakika 90 kukamilika ubao uliposoma Namungo 2-0 Ihefu.

Katika mchezo huo Fikirini Bakari kipa wa Ihefu aliokoa mkwaju wa penalti dakika ya tatu Novemba 23.

 Keneth Kunambi alionyeshwa kadi nyekundu ya mapema zaidi dakika ya pili ya mchezo katika harakati za kuokoa mpira uliokuwa unakwenda nyavuni huku kipa akiwa ametoka.

Mabao ya Pius Busitwa dakika ya 36 na bao la pili lilifungwa na Hamad Majimengi dakika ya 78 yalitosha kuwapa pointi tatu Namungo FC.

Ikumbukwe kwamba Namungo FC ilitoka kupata pointi moja kwenye mchezo wao wa ligi wakiwa ugenini dhidi ya Simba Uwanja wa Uhuru.

Katika mchezo huo ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma Simba 1-1 Namungo na Relliats Lusajo alifunga kwa Namungo na Jean Baleke alifunga kwa upande wa Simba.

Namungo inafikisha pointi 11 ikiwa nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 10 huku Ihefu ikiwa nafasi ya 14 na pointi 8 baada ya kucheza mechi 10.