YANGA KAZI KAZI KUWAKABILI WAARABU

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa mpango kazi mkubwa kwenye mechi yao dhidi ya Waarabu wa Algeria, CR Belouizdad.

Timu hiyo inakibarua cha kuanza kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya makundi Novemba 24 kisha wakimaliza kazi hiyo watarejea Dar kumenyana na Al Ahly Desemba 2.

 Gamondi amesema kuwa kila mchezo ni muhimu kupata ushindani hasa kwenye mechi za kimataifa ambazo ushindani wake huwa mkubwa.

“Kila mchezo una umuhimu kwetu kushinda ipo hivyo na wachezaji wanatambua kwamba kipi ambacho tunahitaji katika kila mchezo ambao tunacheza iwe ni kitaifa ama kimataifa.

“Wapinzani tulionao sio wa kuwabeza, tunawatambua na tunawaheshimu hivyo ambacho tunahitaji ni kuwa kwenye mwendo mzuri na kupata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza,” amesema Gamondi.

Tayari kikosi cha Yanga msafara wa kwanza umewasili Algeria kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo na msafara wa pili unatarajiwa kuwasili leo.

Ni wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya taifa ikiwa ni pamoja na Dickson Job, Bacca hawa walikuwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kwenye msafara wa kwanza ni Zawad Mauya, Kibwana Shomari, Maxi Nzengeli hawa wapo na timu Algeria kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ijumaa.