STARS YAPETA, MTUPIAJI AFUNGUKA

UKIWA ni mchezo wa ugenini kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Novemba 18 ilifanikiwa kupeta na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Bao pekee la mchezo huo wa kwanza kuwania kufuzu Kombe la Dunia limefungwa na Charles M’mombwa dakiak ya 60 akimalizia pasi ya Mbwana Sammata.

Samatta ambaye ni nahodha aliwaongoza wachezaji wa Stars kufanya kweli kwenye mchezo huo muhimu wakiwa ugenini na kufanikiwa kukomba pointi tatu.

Ushindi huo unaifanya Stars kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi E ikiwa na pointi tatu nyuma ya Zambia ikiwa na utofauti wa mabao.

Mchezo unaofuata kwa Stars ni dhidi ya Morocco katika uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 21 saa 4:00 usiku.

Mtupiaji wa bao hilo la ushindi ameweka wazi kuwa ni furaha kubwa kupata ushindi ikiwa ni zawadi kwa Watanzania.