BOSI YANGA ANUNUA KESI YA WAARABU WA SIMBA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hesabu katika Ligi ya Mabingwa Afrika ni kupata pointi tatu kwenye kila mchezo ikiwa ni pamoja na Waarabu wa Misri, Al Ahly.

Ikumbukwe kwamba Al Ahly waliwafungashia virago Simba kwenye African Footbal League kwa faida ya mabao ya nyumbani baada ya mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Simba 2-2 Al Ahly.

Mchezo wa mwisho ulioamua matokeo, Al Ahly 1-1 Simba. Hivyo Simba waliondolewa kikanuni. Al Ahly watakutana na Yanga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa huku wakinunua kesi hiyo kwa kuweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga ameweka wazi kuwa mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Al Ahly utakuwa ni muhimu kwao kupata pointi tatu.

“Tutaingia uwanjani kwa nidhamu kwa kuwa tunakabiliana na mabingwa. Hivyo ambacho tutakifanya ni kuwaheshimu na kucheza nao kwa umakini kupata pointi tatu kwa kuwa wapo ambao walishindwa kupata ushindi mbele yao.

“Katika mashindano haya makubwa kinachoangaliwa ni pointi tatu hilo lipo wazi na wachezaji wanatambua kwamba tuna kazi ngumu ya kufanya kufikia malengo yetu,” amesema Kamwe.