KIMATAIFA SIMBA YATANGAZA WAGENI RASMI NA KAZI KUANZA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika wapo tayari na mashabiki watakuwa ni wageni rasmi kwenye mchezo huo.

Ipo wazi kwamba ni Roberto Oliveira na pira papatupapatu alikiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya makundi kwa sasa hatakuwa na timu hiyo baada ya kusitishiwa mkataba wake.

Mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa ni Novemba 5 2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji kupata matokeo mazuri.

“Tuna mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas. Utachezwa siku ya Novemba 25, 2023 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa. Wageni watawasili Novemba 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31. Waamuzi wa mchezo watatoka nchini Misri.

“Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.”