TAIFA STARS WAANZA KAZI KAMBINI

BAADA ya kuripoti kambini nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameanza rasmi mazoezi kwa ajili ya kuwa fiti kwa mechi za ushindani.

Ni Novemba 11 rasmi walianza mazoezi hayo ikiwa ni kuelekea kwenye mechi mbili ngumu na zitakazokuwa na ushindani mkubwa.

Hizo ni kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger na Morocco.

Mechi ya kwanza kwa timu hiyo ya Tanzania itakuwa ugenini dhidi ya Niger Novemba 18 kisha na Morocco Novemba 21 katika Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni pamoja na Aishi Manula, Kibu Dennis, Bacca, Mzize.