HILI JAMBO KUBWA KUTOKA KWA PROFESSOR JAY

MKONGWE kwenye muziki wa Bongo Fleva, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay anatarajiwa kuzindua jambo kubwa kwa ajili ya jamii hivi karibuni.

Taarifa imeeleza kuwa ni uzinduzi wa Taasisi ya Professor Jay Foundation, unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2023, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Taasisi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa wa figo nchini, huku muasisi wake ambaye ni nguli wa muziki wa kizazi kipya na mbunge wa zamani, Joseph Haule ‘Prof Jay’, akiwaomba wadau mbalimbali wajitokeze kuwachangia.