Home Sports HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOIFUNIKA SIMBA

HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOIFUNIKA SIMBA

MUUNGANO wa nyota watatu ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni Pacome Zouzoah, Aziz KI na Maxi Nzengeli ni dawa tatu ndani ya kikosi hicho kutokana na dozi ambazo wanatoa kwa wapinzani wao.

Mastaa hao watatu wamehusika kwenye mabao 18 kati ya 26 yaliyofungwa na timu hiyo baada ya kucheza mechi 9 ambazo ni sawa na dakika 810. Idadi hiyo ya mabao inafanya muunganiko huo kuifunika Simba jumlajumla kwenye idadi ya mabao.

Ni mabao 17 Simba imetupia baada ya kucheza mechi saba na kinara wao wa kutupia ni Jean Baleke mwenye mabao sita kibindoni akifuatiwa na Moses Phiri mwenye mabao matatu.

Pacome katupia mabao manne, Aziz KI mabao 7 sawa na Nzengeli wakiwa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Weka kando suala la kufunga nyota hao ni watengeneza mipango katika timu ambapo Maxi ana pasi mbili za mabao sawa na Aziz KI huku Pacome akiwa na pasi moja ya bao.

Miamba hiyo kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba Novemba 5 wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga kila mmoja alitupia bao kwenye mchezo huo.

Aziz KI alitupia bao moja, Maxi alitupia mabao mawili huku Pacome akitupia bao moja na lile jingine la ufunguzi lilifungwa na Kennedy Musonda dakika ya tatu ya mchezo huo.

Previous articleLAKINI SIMBA MNA UHAKIKA TATIZO NI ROBERTINHO?
Next articleMKIA UMALIZWE, WACHEZAJI WANALIA NA MENGI