HII HAPA SIRI YA GAMONDI KUMTUNGUA OLIVEIRA ALIYEFUTWA KAZI

MARA baada ya kupata ushindi wa mabao 5-1, Kocha Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi, ameibuka na kutaja siri tatu ya ushindi huo kwa timu yake.

Timu hizo zilivaana juzi Jumapili katika mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ukiwa ni wa Ligi Kuu Bara.

Gamondi alianza kwa kuwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma na kutimiza majukumu aliyowapa kabla na wakati mchezo.

Gamondi alitaja siri tatu ambazo ziliwapa ushindi huo, moja ni nidhamu ya uchezaji kwa wachezaji wake wanapokuwa na mpira na wanapoupoteza katika kukaba na kusababisha mpinzani kushindwa kumiliki kwa muda mrefu.

Aliitaja ya pili, vipaji walivyonavyo wachezaji ambavyo vimeamua matokeo hayo wakiongozwa na Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Stephane Aziz Ki.

Alimalizia ya tatu ni morali ya kila mchezaji ya kutaka kupata ushindi katika kila mchezo, ambayo anaamini wakiendelea nayo itafikia malengo yao ya msimu huu huku akiwataka wachezaji wake kutobweteka baada ya ushindi.

Rasmi Novemba 7 2023 Simba imefikia makubaliano ya kuachana na Roberto Oliveira ambaye alikuwa kwenye benchi timu hiyo ikikutana na kipigo hicho kikubwa.