YANGA NA SIMBA ZAKOMBA TUZO

WAKATI ikiwa ni presha ya kuelekea Kariakoo Dabi inayotarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 5 2023 Yanga na Simba zimesepa na tuzo.

Ni tuzo ya mchezaji bora ambayo imekwenda Yanga kwa nyota Aziz KI akiwashinda wachezaji wenzake alioingia nao fainali ikiwa ni Maxi Nzengeli wa Yanga na Moses Phiri wa Simba.

KI kwa Oktoba alikuwa kwenye ubora wake na aliwafunga Azam FC hat trick kwenye mchezo wa Mzizima Dabi.

Kwa upande wa Simba ni Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kakomba tuzo ya kocha bora Oktoba.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi imeeleza kuwa Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) imemchagua Oliveira kuwa Kocha Bora wa Oktoba 2023 baada ya kuwashinda Miguel Gamondi wa Yanga na Abdihamid Moallin wa KMC ambao aliingia nao fainali ya mchakato wa tuzo hizo.