KABATI la Lionel Messi raia wa Argentina limekusanya jumla ya tuzo kubwa za Ballon d’Or 8 baada ya kutwaa kwa mara nyingine tena usiku wa Jumatatu tuzo yake.
Nyota huyo kabla ya kuibukia Inter Miami msimu huu alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kutwaa taji la Kombe la Dunian Qatar na alitupia mabao mawili kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa.
Ni mabao 32 alifunga kàtika mechi 55 za mashindano yote akiwa na PSG ambao walitwaa taji la ligi pia.
Messi ametwaa tuzo hiyo akiwashinda wapinzani wake wa karibu ambao ni Erling Haaland ambaye ni namba mbili, Kylian Mbappe namba tatu na Kevin De Bruyne ambaye amegotea namba nne.