WIKI ya 10 ndani ya Premier League, Manchester United wamechapwa kwenye Dabi na kupoteza pointi tatu dhidi ya Manchester City.
Nyumbani walikuwa Uwanja wa Old Trafford walishuhudia ubao ukisoma Manchester United 0-3 Manchester City.
Mwamba Erling Haaland alitupia mabao mawili dakika ya 26 na 49 huku Phil Foden akitupia bao moja usiku dakika ya 80.
Manchester City namba tatu pointi 24 kibindoni huku Manchester United ikiwa nafasi ya 8 pointi 15 kibindoni.
Manchester United ya Onana bado hawajaonana kwenye msako wa pointi tatu wakipata tabu kwenye msako wa ushindi.