RIPOTI mbaya haipendezi kwa anayeipata ajabu yule anayesababisha hayo yatokee kwake ni burudani kupata kile ambacho alikuwa anakitaka mwisho wa mchezo huku kukiwa na mtu ambaye alipigwa na kitu kizito.
Singida Fountain Gate hawakuwa na bahati kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga walipopoteza pointi tatu muhimu Uwanja wa Mkapa ilikuwa Oktoba 27 2023.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-0 Singida Fountain Gate hapa tunakuletea baadhi ya kazi ilivyokuwa kwa mastaa wote namna hii:-
Djigui Diarra
Alipiga pasi ndefu dakika ya 9, 13, 61 aliokoa hatari dakika ya 89. Dakika 90 alikomba bila kufungwa kwenye mchezo huo.
Yao
Yao Attohoula alipiga pasi ndefu dakika ya 74, alicheza faulo dakika ya 59, alipiga pasi fupi dakika ya 5, 23, 56, 62, 74, 77. Alitoa pasi ya bao dakika ya 36 kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18. Alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 40 aliokoa hatari dakika ya 45.
Pacome
Pacome Zouzoua alipiga pasi fupi dakika ya 7, 38, 45, alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 7, 33 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 18. Alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 27. Alichezewa faulo dakika ya 69.
Mudathir
Mudhathir Yahya alipiga pasi fupi dakika ya 7, 9 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 10, alipiga pasi ndefu dakika ya 27, 35.
Job
Dickson Job alichezewa faulo dakika ya 50 aliokoa hatari dakika ya 7, 33. Alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 14.
Nondo
Bakari Nondo Mwamnyeto aliokoa hatari dakika ya 36, 38, 84, 90 alicheza faulo dakika ya 24 na aliokoa hatari dakika 90, miongoni mwa pasi ndefu ambazo alipiga ilikuwa dakika ya 13.
Aziz
Aziz KI alipiga pasi fupi dakika ya 10, 24, 61 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 25, 62. Dakika ya 14, 56 alipiga faulo, alicheza faulo dakika ya 29, 34 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 54.
Lomalisa
Joyce Lomalisa alimwaga krosi dakika ya 12, 33, 54 aliokoa hatarai dakika ya 17, 25.
Maxi
Maxi Nzengeli alipiga pasi fupi dakika ya 23, 24, 53, 56, 74, 85, alipiga pasi ndefu dakika ya 25, 38, 89. Alifunga mabao mawili namna ya 30 na 38.
Konkoni
Hafiz Konkoni alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 15, 56, alichezewa faulo dakika ya 15, 17, 69 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 56 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 45.
Singida Fountain Gate
Benedict Haule alianza kikosi cha kwanza alitunguliwa mabao mawili dakika ya 30 na 38. Aliokoa hatari dakika 7, 15, 27, 32 alipiga pasi ndefu dakika ya 11 alikomba dakika 44 baada ya kupata maumivu nafasi yake ilichukuliwa na Ibrahim Rashid, (Parapanda) aliyeokoa hatari dakika ya 75, 88,89.
Bruno Gomes alipiga pasi fupi dakika ya 8, 15, 45, aliokoa hatari dakika ya 44, 45 alichezewa faulo dakika ya 52.
Yahya Mbegu aliokoa hatari dakika ya 20, 25, 66.
Habib Kyombo alichezewa faulo dakika ya 8 alipiga krosi dakika ya 21.
Yusuph Kagoma aliokoa hatari dakika ya 12, 29, 86, 89, alicheza faulo dakika ya 4, 55 alionyeshwa kadi ya njano.
Kelvin Kijili alipiga krosi dakika ya 13, 63, 79, 90, aliokoa hatari dakika ya 52, 66, 86.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, (Dizo Click).