YANGA WAKOMBA POINTI ZA SINGIDA FOUNTAIN GATE

YANGA imekomba pointi tatu mazima mbele ya Singida Fountain Gate kwenye mchezo wa ligi uliokuwa na ushindani mkubwa hasa kipindi cha pili.

Ni mchezo wa ligi ikiwa ni mzunguko wa 7 kwa msimu wa 2023/24.

Chuma cha kwanza ilikuwa dakika ya 30 na kile cha pili dakika ya 38 yalidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Dakika 45 za mwanzo Singida Fountain Gate walikuwa wakicheza kwa kujilinda huku Yanga wakipeleka mashambulizi yaliyowapa faida na kukomba pointi tatu.

Nafasi ya kwanza kwenye msimamo na kibindoni wana pointi 18 baada ya kucheza mechi saba mchezo ujao ni dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Novemba 5 2023.