Home Sports UNA HELA? WIKIENDI IPO BIZE KINOMANOMA

UNA HELA? WIKIENDI IPO BIZE KINOMANOMA

UKIWA unajua wapi unakwenda ni rahisi kufika hata ukikutana na vikwazo vingi, lakini swali la msingi kujiuliza una hela? Ijumaa ipo bize utatokaje sasa nje ama ndani?

Kwenye ulimwengu wa mpira, kuna mechi kali zinatarajiwa kuchezwa leo katika msako wa pointi tatu muhimu.

Hapa tunakuletea namna msako wao utakavyokuwa:-

Yanga v Singida Fountain Gate

Ngoma inapigwa Uwanja wa Mkapa saa 12:15 utakuwa ni msako wa pointi tatu za jasho kwa wanume 22 ndani ya uwanja kuonyeshana ubabe.

Ladha ya ushindi

Timu zote mbili zimetoka kuonja ladha ya ushindi kwa kukomba pointi tatu. Yanga wao walikuwa nyumbani kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ubao ulisoma Yanga 3-2 Azam FC, pointi zikabaki mikononi mwa Wananchi. Singida Fountain Gate walikomba pointi tatu ugenini. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 2-3 Singida Fountain Gate.

Mfanano wa ushindi kwa timu hizi mbili unanogesha mechi ya leo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Milima haikutani

Deus Kaseke kiraka ndani ya Singida Fountain Gate aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Yanga.Kwa sasa yupo ndani ya Singida Fountain Gate. Beno Kakolanya kipa wa Singida Fountain Gate aliwahi kucheza ndani ya Yanga kisha akaibukia Simba na sasa anakutana na mabosi wake wa zamani.

Mbrazil na Muargentina

Miguel Gamondi yeye yupo ndani ya kikosi cha Yanga ni raia wa Argentina. Mbinu zake zilijibu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Msenegal, Yusuph Dabo wa Azam FC.

Singida Fountain Gate ipo chini ya kocha mpya ambaye ni raia wa Brazil anaitwa Ricardo Ferreira. Mchezo wake wa kwanza kukaa benchi ilikuwa dhidi ya Namungo walipokomba pointi tatu ugenini.

Utupiaji ni balaa Yanga

Safu ya ushambuliaji ya Yanga ina balaa kwenye utupiaji mabao ndani ya ligi. Baada ya kucheza mechi sita imetupia mabao 18 na ukuta wao umeruhusu mabao manne.

Singida Fountain Gate ni mabao sita safu yake ya ushambuliaji imetupia sawa nay ale waliyotunguliwa ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 90 baada ya kucheza mechi sita.

KMC v Tanzania Prisons

Wakusanya mapato wa Kinondoni, KMC wanawakaribisha Wajejela, Tanzania Prisons kutoka Mbeya kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.

Oktoba 22 ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma Tabora United 0-0 KMC hivyo waligawana pointi mojamoja ugenini leo watakuwa nyumbani.

Prisons Oktoba 22 ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Prisons 1-1 JKT Tanzania nao walikomba pointi moja wakiwa nyumbani, leo watakuwa ugenini.

Azam FC v Namungo

Hasira zao za kupoteza mechi zilizopita zinakwenda kukutana ndani ya Uwanja wa Azam Complex. Ni Azam FC walipoteza dhidi ya Yanga na Namungo walipoteza dhidi ya Singida Fountain Gate.

Namungo kwenye ushambuliaji kuna tabu baada ya mechi sita ni mabao manne walitupia huku Azam FC ikiwa ina mabao 12.

Ukuta wa Azam FC ulitunguliwa mabao matano na Namungo ni mabao 7 kazi itakuwa nzito leo, una hela? Wikiendi ipo bize kinomanoma.

Previous articleUNAKUWAJE MJANJA KAMA HUJABASHIRI NA MERIDIANBET WIKENDI HII?
Next articleJESHI LA YANGA HILI HAPA DHIDI YA SINGIDA FOUNTAIN GATE