WILLY Onana nyota wa Simba yupo kwenye mtego ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kwa kutakuwa kutumia nafasi zinazopatikana kwenye mchezo.
Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa African Football League leo Ijumaa dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa huku Onana akiwa ni miongoni mwa nyota waliopo kwenye mpango kazi wa kocha huyo.
Mbali na Onana, Moses Phiri,Luis Miquissone, Kibu Dennis ni miongoni mwa nyota waliokuwa kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo.
Oliveira amesema kuwa wachezaji wake wote ni muhimu kutumia nafasi wanazopata uwanjani kupata ushindi kwa kuwa ni mara chache zinatengezwa.
“Nafasi kwenye mechi za kimataifa ambazo zinatengenezwa huwa ni chache hivyo zikipatikana ni muhimu kuzibadili kwa kufunga hilo ni jambo kubwa na tunalifanyia kazi kila wakati.
“Ukweli ni kwamba wachezaji waliopo wana uwezo mkubwa na wananifurahisha namna ambavyo wanapokea maelekezo na kuyafanyia kazi nina amini tutafikia malengo yetu,”.