MTIBWA Sugar ikiwa Uwanja wa Manungu imeshuhudia Oktoba 19,2023 ubao ukisoma Mtibwa Sugar 0-2 Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ni Sugar Dabi.
Mambo ni magumu kwa timu hiyo kutokana na mwendo wake kuwa ni wa kusuasua msimu mpya wa 2023/24 kwenye mechi za mwanzo.
Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa kwa awamu kila kipindi bao moja dakika ya 30 na All Nassoro na kipindi cha pili limepachikwa bao na Said Omary dakika ya 90.
Unakuwa ni mchezo wa sita kwa Mtibwa Sugar kushuka uwanjani msimu wa 2023/24 bila kuambulia ushindi.
Inabaki na pointi zake mbili kibindoni baadaya kucheza mechi sita za ligi huku Kagera Sugar ikifikisha pointi 8 nafasi ya sita kwenye msimamo na Mtibwa Sugar ni nafasi ya 16.