JEMBE AWEKA REKODI HII FIFA

MHARITI Mtendaji wa Group Group, Saleh Ally, maarufu kama Salehjembe, ameandika rekodi nchini ya kuwa mwandishi wa kwanza kupiga kura mara nne mfululizo katika tuzo za The Best FIFA Football Award.

Hali hiyo inaoonyesha uaminifu mkubwa kutoka Fifa yenye makao yake makuu nchini Uswiss.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limemchagua kwa mara nyingine tena Salehjembe, kupiga kura katika tuzo za mwaka 2023 ambazo hutoa mwanasoka bora wa dunia.

Kawaida katika kila nchi hutolewa nafasi kwa kocha wa timu ya taifa, nahodha wa timu ya taifa na waandishi wa habari kupiga kura hizo muhimu.

Kura atakazopiga ni vipengele sita vya The Best FIFA Women’s Player, The Best FIFA Women’s Coach, The Best FIFA Women’s Goalkeeper, The Best FIFA Men’s Player, The Best FIFA Men’s Coach na The Best FIFA Men’s Goalkeeper.