UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa bado ligi ni mbichi wana muda wa kuendelea kupambana katika kutimiza malengo yao ya kutwaa ubingwa.
Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wa taji la ligi baada ya kutwaa msimu wa 2022/23. Ipo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Gamondi baada ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi tano ni shuhuda akipoteza mchezo mmoja aliposhuhudia ubao wa Uwanja wa Highland Estate ukisoma Ihefu 2-1 Yanga.
Mchezo dhidi ya Geita Gold uboa ulisoma Geita Gold 0-3 Yanga wakakomba pointi tatu mazima.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa bado wana muda wa kuendelea kufanyia kazi makosa na kupata matokeo kwenye mechi zinazofuata.
“Kupoteza mchezo mmoja haina maana kwamba tumepoteza kila kitu hapana. Ni wapinzani walikuwa bora wakapata matokeo kwenye mchezo ambao tulikuwa tunahitaji matokeo mazuri.
“Bado mbio zinaendelea kwani kuna mechi 30 ambazo zitakamilisha mzunguko wa kwanza na wa pili. Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” alisema Kamwe.