TANZANIA Prisons, (Wajelajela) leo Oktoba 5 wanatarajia kuwapigisha kwata Simba Kwa kuwachezea pira gwaride mguu pandeeeee.
Chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro Prisons ameweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu.
Mchezo huo ni wa mzunguko wa nne ambapo Simba itakuwa ugenini ukiwa ni mchezo wake wa pili.
Mchezo wa kwanza Simba kuwa ugenini ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar na ilishuhudia ubao ukisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba.
Mchezo uliopita kwa Prisons ilikuwa ugenini dhidi ya Azam FC ilishuhudia ubao ukisoma Azam FC 3-1 Prisons.
Minziro amesema: “Tunajua tuna mchezo dhidi ya Simba ambao utakuwa mgumu, kikubwa ni maandalizi mazuri kupata matokeo mazuri.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi tupo tayari kupata ushindi na tunaamini kila kitu kinawezekana,”.