KUTOKANA na kikosi cha Simba kucheza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika mpira papatupapatu, Kocha Mkuu wa Simba Robert Oliveira ameweka wazi kuwa watafanya vizuri.
Kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Power Dynamos ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba na mabao ya Simba ni Clatous Chama alifunga.
Ule wa pili ubao ulisoma Simba 1-1 Power Dynamos ambapo ni Kondwani Chidon alijifunga.
Leo, Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
“Sikiliza, mpango ni kupata matokeo na kucheza soka la kuvutiana tunaweza kufanya hivyo kutokana na wachezaji tulionao kwenye kikosi,”.