BANGALA MAJANGA AZAM FC

NI Yannick Bangala kiungo wa Yanga hatakuwa kwenye mchezo ujao wa timu hiyo dhidi ya Coastal Union, Oktoba 6 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Bangala amechanika msuli wa nyuma ya paja, kwenye mchezo wa jana Jumanne dhidi ya Dodoma Jiji.

Baada ya mechi hiyo, Bangala alirudi Dar Es Salaam kwa vipimo zaidi, wakati timu ikielekea Tanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya Coastal Union, Oktoba 6.

Baada ya vipimo ndiyo itajulikana ukubwa wa tatizo na muda wa matibabu hadi kupona.