HAWAAMINI macho yao Power Dynamos wapinzani wa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushuhudia wakipokwa tonge mdomoni la kutinga hatua ya makundi.
Kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Power Dynamos walianza kuwatungua Simba ndani ya dakika 20 za mwanzo kipindi cha pili mambo yalibadilika na kuruhusu nyavu zao kutikishwa.
Dakika 90 zilikamilika Simba 1-1 Power Dynamos, Simba inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya mchezo uliochezwa Zambia ubao kusoma Power Dynamos 2-2 Simba.
Hapa tunakuletea namna kazi ilivyokuwa namna hii:-
Ayoub Lankerd
Aliokoa hatari dakika ya 23, 48, 49, 76. Alipiga pasi ndefu dakika ya 14, 56, 71, 73, 76, 77, 86 na alipiga pasi fupi dakika ya 20, 25, 28, 31, 45 alioyeshwa kadi ya njano dakika ya 90.
Ni bao moja alitunguliwa dakika ya 16 na Andy Boyal aliyekuwa nja ya 18. Bayal alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 77 na alipiga mashuti yaliyolenga lango dakika ya 49, 76.
Kapombe
Shomari Kapombe alipiga faulo dakika ya 38, alipewa jukumu la kurusha dakika ya 18, 41, 52, 80, 83 alipiga pasi ndefu dakika ya 21, 28, 31, 45, 52, 58, 79, 80, 88.
Mohamed Hussein
Alipiga pasi ndefu dakika ya 50, 84 aliokoa hatari dakika ya 27, 43 pasi fupi alipiga dakika ya 29, 33, 38, 39 alicheza faulo dakika ya 32 alichezewa faulo dakika ya 57.
Kennedy Juma
Juma alipiga pasi ndefu dakika ya 50, 66 alipiga pasi fupi dakika ya 28, 29 alikomba dakika 90.
Che Malone
Malone aliokoa hatari dakika ya 19, 28, 29, 85, alipiga pasi fupi dakika ya 25, 26, 42, 72, 84.
Mzamiru Yassin
Mzamiru alikomba dakika 58 nafasi yake ilichukuliwa na Willy Onana aliyepiga shuti lililolenga lango dakika ya 74 na lile ambalo halikulenga lango dakika ya 59.
Mzamiru alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 20, aliokoa hatari dakika ya 20 na alimwaga krosi dakika ya 32.
Ngoma
Fabrice Ngoma ni dakika ya 23, 39 alitoa pasi ndefu dakika ya 73 alipiga pasi ndefu na alikomba dakika 90.
Chama
Clatous Chama alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 25, 62, 78, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 70 alichezewa faulo dakika ya 25, alipiga kona dakika ya 36.
Majukumu ya kona kwa Power Dynamos yalikuwa kwenye miguu ya Joshua Mutale aliyepiga kona dakika ya 24, alichezewa faulo dakika ya 32.
Baleke
Jean Baleke alikwama kusepa na dakika 90 baada ya kupata maumivu ya mguu dakika ya 40, alipiga mashuti ambayo yalilenga lango dakika ya 34, 35 na kipa Williad Mwanza aliokoa hatari hizo.
Alitumia dakika 45 Baleke nafasi yake ikachukuliwa na John Bocco, alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 53, 88 alipiga krosi dakika ya 69 ikatemwa na Mwanza kisha ikagotea kwenye miguu ya Kondwani Chidoni aliyejifunga katika harakati za kuokoa.
Pia Chidoni alionyeshwa kadi ya njano dakika 26.
Ntibanzokiza
Saido Ntibanzokiza alipiga kona dakika ya 18, 88 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 42, 65 alicheza faulo dakika ya 61, 77 na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 44.
Kibu
Kibu Dennis alipiga pasi fupi dakika ya 29, 33 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 55 alikomba dakika 74 ni Sadio Kanoute aliingia kukamilisha ngwe ya mwisho.