MAOKOTO Deilee yanazidi kupasua anga huku washindi wakizidi kukomba zawadi zao kila baada ya droo kufanyika.
Leo Oktoba 2 watatu wamesepa na zawaid zao baada ya kushinda.
Ni Mwinyi Milevu na Fednand Kisanga hawa walishinda simu huku mshindi mmoja akikomba zawadi ya fedha taslimu.
Anaitwa Yassin Mfalla kashinda milioni moja ambayo ni zawadi kwake kwa kushiriki Maokoto Deilee.
Hivi karibuni washindi watatu Yasinta Kilumule (Njombe), Emmanuel Ngusa(Dumila), walisepa na simu janja.
Tumaini Kajela, (Songwe) amejishindia shilingi 1,000,000, katika droo ya Tano ya wiki ya Maokoto Deilee kutoka Tigo pesa na SportPesa.
Droo hii ni sehemu ya promosheni ya Maokoto Deilee iliyoandaliwa na SportPesa kwa kushirikiana na Tigo Pesa, na pia ni muendelezo wa zawadi ambazo zinatolewa kila siku kwa washindi 10 ambao hujishindia kiasi cha TZS 20,000.
Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa kwenye viwanja vya Tegeta Nyuki, Jijini Dar-Es-Salaam, Ofisa wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Lydia Solomon alisema droo ya Tano katika promosheni ya Maokoto Deilee ilipochezwa wateja wa Tigo pesa na SportPesa walijishindia simu janja na shilingi milioni 1.
‘’Kama mnavyofahamu droo yetu ya tano ya Maokoto Deilee, ambapo wateja watatu kutoka Njombe, Dumila na Songwe, wameshinda simu janja na shilingi milioni moja kwa mmoja, baada ya kubashiri na na kuibuka washindi wa Maokoto Deilee ya Sportpesa na Tigo pesa.
Akiongea kwa niaba ya Tigo, Meneja Biashara wa Tigo pesa Keneth Ndulute, alisema wachezaji wa SportPesa ambao wanatumia laini za simu za Tigo hawana budi kuiga mfano wawenzao ambao wameshinda kwa kucheza na kuingia kwenye droo ili na wao washinde.
‘’Ninapenda kuwahamasisha watanzania wenzangu hususani wateja wetu wa Tigo pesa kuchangamkia fursa hii. Nitoe rai kwa wateja wetu kuendelea kushiriki na kucheza promosheni hii ambayo imebakiza takribani wiki mbili.
Ili kuweka bashiri yako kupitia TigoPesa, wateja wanaweza kupiga *150*87# kuchagua namba 4, na kuweka kiasi anachotaka, kisha kuweka PIN yako ya Tigopesa ili kukamilisha muamala.
“Kwa wale ambao hawakushinda wasikate tamaa kwani promosheni bado inaendelea kila siku hivyo waendelee kucheza.”
Ikumbukwe promosheni hii ilizinduliwa rasmi siku ya Agosti 21 ya wiki iliyopita inajumuisha zawadi za shilingi elfu 20 kila siku, zawadi za milioni moja moja kwa mshindi mmoja kila wiki, simu janja kwa washindi wawili kila wiki na zawadi ya milioni 15,000,000 siku ya kufunga kampeni.